
Maswali kumi ya kuchochea fikra nzito
Mahitaji ya data ambazo ni sahihi yametiliwa mkazo mkubwa. Haijawahi kutokea hapo
kabla kwa Hazina kuhitaji data kama ilivyo sasa. Baada ya Programu ya urekebishaji wa
uchumi pamekuwa na mahitaji makubwa ya kupata na kufafanua data za umasikini na maisha
bora (Mkurugenzi wa Kitengo cha Taifa cha Takwimu).
Tutumie muda gani na kwa gharama gani kupata taarifa?
Makanisa yanashirikiana na serikali katika kushughulikia suala la rushwa, ikiwa
pamoja na kuendesha mikutano kuhusu jinsi ya kuendeleza uwazi. Jambo hili ni muhimu ili
watu na wafadhili waone kuwa misaada na kufutiwa madeni vinawanufaisha watu masikini
(Archbishop Donald Mtetemela)
Je, jambo la rushwa linaweza kukabiliwa vipi zaidi?
Kupandisha kodi ni kitu kisichopendwa na baadhi ya kodi ni mzigo mkubwa kwa watu
masikini kuliko watu matajiri
Je, serikali ikusanye kodi zaidi kutoka kwa watu ili kuhakikisha upunguzaji wa
umasikini?
Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia hawajatimiza ahadi zao za kutathmini
athari za mageuzi yaliyopendekezwa katika programu zao kabla ya kuzikubali. Kwa sababu ya
kukosa taarifa ya athari, katika nchi nyingi, hakuna hadi sasa, majadiliano ya maamuzi ya
sera. (OXFAM).
Je, sekta muhimu na vipengele vyake vilivyochaguliwa katika mpango wa kupunguza
umaskikini Tanzania (PRSP) ni bora kuliko vinginevyo?
Mifumo ya aina mbili ya elimu na afya imeanza kutokea Tanzania. Watu tajiri na
watoto wao wanaenda katika shule binafsi za gharama kubwa na hospitali aghali za binafsi
wakiacha watu masikini kutumia huduma duni za jamii ambazo zinapewa fedha kidogo
(TGNP)
Je, mpango wa Kupunguza Umasikini Tanzania unaonaje mfumo huo wenye uwili?
Bei ya mazao imeshuka, pembejeo zinapanda na pembejeo muhimu ama hazipatikani au
hazipatikani kwa wakati unaotakiwa. Akiba ya Chakula ya Taifa ipo mashakani kwa sababu ya
biashara huru na athari zake hasa kwa wazalishaji wa chakula. Athari yake ni mbaya zaidi
kwa wakulima wadogo wadogo hasa wale wa kusini na magharibi mwa nchi, sehemu ambazo
zilikuwa zinalisha Taifa. Aidha wafugaji wamepuuzwa na kusahauliwa kabisa na sera
hizi. (TGNP)
Je, mpango wa Kupunguza Umasikini Tanzania kama ulivyo unashughulikia tatizo hili la
Akiba ya Chakula?
Takwimu zinaonyesha kuwa katika mpango wa Upunguzaji Umasikini Tanzania kuna
pengo la fedha. Mahitaji ya fedha na fedha halisi zilizotengwa za matumizi mengine na
matumizi ya maendeleo kwa ajili ya sekta sita muhimu (elimu, afya, maji, sheria, kilimo na
barabara) yaonyesha kuwa kuna uwezekano wa asilimia 54% kwa mwaka 1999/2000, 69% mwaka
2000/2001, 75% mwaka 2001/2002 na aslimia 86% katika mwaka wa 2000/2003. Kwa hiyo hakuna
fedha asilimia 100% kwa kutekeleza Mkakati wa Upunguzaji umasikini Tanzania (PRSP) kwa
miaka mitatu ijayo (TASOET)
Je, pengo hilo la fedha litashughulikiwa vipi?
Majadiliano Bungeni kuhusu Mpango wa Upunguzaji Umasikini Tanzania yalichukua
muda wa masaa mawili tu. Kwa kuzingatia umuhimu wa waraka kwa ajili ya kufikia malengo na
matendo yaliyowekwa katika Mbinu ya Ufutaji Umasikini Kitaifa (NPES), inatia wasiwasi kama
kweli muda ulitosha ili kufikia uamuzi wa pamoja wa kisiasa katika utelelezaji wa waraka
huo. (Evans, Nglawea na Semboja, Novemba 2000)
Tufanye nini ili kufikia uamuzi wa pamoja wa kisiasa?
Kipengele cha umilikaji cha Mpango wa Upunguzaji wa Umasikini (PRSP) ambacho kinahitaji
kueleweka vizuri ni matendo au vipengele vinavyobainisha kazi za jumuiya katika mpango
huo. (TASOET)
Je, tunawezaje kuhusisha yale yanayopaswa kutekelezwa na serikali na yale yanayopaswa
kutekelezwa na watu kwa kuwa jambo hili ni muhimu katika kukuza dhana ya umilikaji?