
Dibaji
Imeelezwa katika Mkakati wa upunguzaji Umasikini (PRSP) kwamba "Serikali
inakusudia kuendelea kuhimiza uwakilishi kamili wa watu masikini na washika dau wengine
katika kutekeleza, kusimamia na kutathmini mbinu za upunguzaji umasikini".

Kijitabu hiki kilichoeleza mkakati huu kwa lugha rahisi ni mchango wa mawazo kutoka
jumuiya za wananchi yaliyoratibiwa na Hakikazi Catalyst. Hakikazi Catalyst ni mojawapo wa
mashirika yaliyopo kwenye mtandao wa kupunguza madeni na kuhamasiaha maendeleo (TCDD).
Nakala elfu tano za Kiswahili na elfu mbili za Kiingereza zimetolewa kwa Serikali kuu,
Mikoa, Wilaya na Jumuiya huru za Wananchi. Mawazo yaliyomo katika kijitabu hiki yanabaki
kama yalivyo katika mkakati wa awali wa serikali (Toleo la Novemba 2000) isipokuwa picha
za kuchorwa (katuni) na vidokezo vilivyoongezwa pamoja na sehemu ndogo inayoeleza baadhi
ya maana ya maneno muhimu. Aidha, kumeongezwa maswali kumi yanayochochea jamii kufikiri
kwa makini kuhusu jitihada za kuondoa umaskini. Ziada hizi zitamsaidia msomaji kuelewa
vizuri kijitabu hiki.
Tumeomba nafasi katika magazeti ya Daily News na Majira kutoa mchango huu katika mwezi
wa Mei na Juni 2001 mara moja kwa wiki ili kupata maoni, majibu na uchambuzi wa upunguzaji
wa umasikini kwa ujumla kutoka kwa watu mbalimbali. Maoni hayo yatanakiliwa katika mtandao
(website, - angalia chini.)
Unakaribishwa kama mtu binafsi au kikundi kutoa maoni yako kuhusu maswali yaliyoulizwa
katika kijitabu hiki na kutoa ushauri unaoona unafaa. Maoni yatumwe kwa: