
Malengo, shughuli na Viashirio
Inasemekana kuwa kama hujui uendako basi barabara yoyote itakufikisha. Watu
ambao hutekeleza mambo wanayoyataka wana mwelekeo sahihi wa kitu wanachotaka kufanya,
watakifanya vipi, na hasa, jinsi watakavyofahamu kuwa wamefaulu.
Lile lililo kweli kwa mtu binafsi ndilo lililo kweli kwa jamii, katika nyanja
mbalimbali na kwa serikali. Kama uko makini kutenda jambo basi lazima uwe wazi kuhusu
malengo, shughuli na viashirio.
| MALENGO |
Wazo lililo wazi kwa lile unalotaka kulifanya litakusaidia kuamua
utalitekeleza kwa kiwango gani na muda wa kukamilika. |
| SHUGHULI |
Wazo lililo wazi kuhusu shughuli utakayotekeleza litakusaidia kuorodhesha
hatua mbali mbali za kufuata |
| VIASHIRIO (DALILI) |
Wazo lililo wazi kuhusu utakachopima litakusaidia kujua shughuli
zinazotekelezwa zinafikia lengo au kuvuka. |
Sehemu hii inaorodhesha malengo, shughuli na viashirio ambavyo vimebainishwa kwa mawazo
yanayoongoza katika Mkakati wa Kuondoa Umasikini (PRSP) ambazo ni:
 | Kupunguza umasikini wa mapato |
 | Kuendeleza ubora wa maisha na ustawi wa jamii |
 | Kupunguza madhara yanayoweza kuwapata watu masikini |
Kwa ujumla njia ya kupunguza umasikini wa mapato ni kuziwezesha shughuli za kuzalisha
mapato ya aina mbalimbali zistawi ili pawe na kazi nyingi zaidi na fedha nyingi ziwepo
kwenye mzunguko. Njia ya kuendeleza ubora wa maisha na ustawi wa jamii ni kuhakikisha kuwa
watu wote wanapata nafasi sawa ya kupata elimu, afya bora, maji salama na chakula bora.
Njia ya kwanza ya kupunguza madhara ni kuainisha watu ambao wako katika hali mbaya na
kugundua matakwa yao ni yapi na kuweka bayana malengo, shughuli na viashirio.
Kupunguza Umasikini wa Kipato
Kama nchi kwa ujumla ingekuwa tajiri zaidi basi panatakiwa pawe na umasikini mdogo. Kwa
hiyo inabidi tuifanye nchi iwe tajiri zaidi na tuhakikishe kuwa utajiri huo unagawanywa
sawasawa na kwa haki. Aidha, makundi ya watu dhaifu wanaoathirika na mabadiliko ya hali ya
kiuchumi walindwe kwa utaratibu wa tofauti.
Mpango wa miaka mitatu ijayo ni kuongeza mapato zaidi kutokana na sekta za kilimo, na
viwanda na huduma.
Mpango huu utawezekana kwa sababu ya mabadiliko yanayofanywa na serikali ya kuweka
mazingira bora na uchumi imara.
Tukichukulia kuwa uchumi mpya unawafikia watu masikini zaidi basi tutakuwa tumepiga
hatua ya kupunguza umasikini.
Malengo
| |
Hadi 2003 |
Hadi 2010 |
| Kupunguza sehemu ya idadi ya watu fukara |
Toka 48-42% |
Toka 48-24% |
| Kupunguza idadi ya watu masikini wa vijijini |
Hadi kufikia 7.5% |
Toka 57-29% |
| Kupunguza idadi ya watu masikini wa chakula |
Hadi kufikia 3.5% |
Toka 27-14% |
Shughuli
Shughuli ambazo ziatapunguza umasikini wa mapato zinaelezwa katika kurasa zifuatazo:
 | Kukuza maendeleo vijijini na kukua kwa biashara ya nje |
 | Kusaidia kukuza sekta binafsi |
 | Kufanya kazi kwa ajili ya kuboresha na kutoa madaraka zaidi ya serikali |
 | Kuhakikisha kuwa uchumi unaimarika |
Viashirio
 | · Kupungua kwa umasikini wa chakula |
 | · Kupungua kwa umasikini wa mahitaji muhimu |
 | · Kupata na kumiliki vifaa kama redio, jokofu (friji), televisheni, n.k. |
 | · Kupata na kutumia vifaa vya kisasa katika ujenzi wa nyumba. |
Maendeleo Vijijini na Ukuaji wa Biashara ya nje
Tanzania ina historia ndefu ya maendeleo vijijini. Juhudi za mwanzo zilidhibitiwa na
taifa na kusaidiwa na mfumo mzima wa serikali kwa wazalishaji wa vijijini. Baadaye juhudi
zilitawaliwa na nguvu za soko huria, huku serikali ikijiondoa polepole. Njia iliyo bora
zaidi haijaeleweka. Katika miaka mitatu ijayo Serikali itamwomba kila mmoja kufanya kazi
kwa ushirikiano ili kutafuta ufumbuzi na kuendeleza Mbinu za Maendeleo Vijijini.
Watu masikini na wafanya biashara binafsi wataombwa kuwa mstari wa mbele katika
kutafuta njia mpya za kufaa na madhubuti.
Malengo na Shughuli
 | Mikopo itatokana na kwa wanunuzi wa mazao, benki na vyama vya ushirika badala ya kutoka
serikalini |
 | Wakulima watajisimamia wenyewe katika makundi au vyama vya ushirika ili kurahisisha
kupata mikopo toka katika taasisi za fedha |
 | Wakulima watashirikishwa kufanya utafiti wa mazao na shughuli nyinginezo ili kuongeza
wingi na ubora wa mazao |
 | Wanunuzi binafsi wa mazao wataendelea kutumia mpango wa vocha na mipango mingine ili
kurahisisha ununuzi wa mbolea na dawa za kuulia wadudu |
 | Jamii zitajishighulisha zaidi katika ujenzi na ukarabati wa barabara za vijijini na
kuendeleza kilimo cha umwagiliaji maji (panapowezekana kwa msaada wa serikali) |
Serikali itajishughulisha tu na kutengeneza sera za kuwasaidia wananchi wa vijijini kwa
kutekeleza yafuatayo:
 | Kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali, benki za ndani na Washirika wa Kimataifa
katika kutoa mafunzo na mifumo mingine ya misaada kwa jumuiya na makundi kuhusu: |
 | Utaratibu wa stadi za uongozi na fedha |
 | Kutengeneza na kukarabati barabara vijijini |
 | Kuendeleza kilimo cha umwagiliaji |
 | Kuweka mazingira yatakayoendeleza shughuli ndogo ndogo na za kati za biashara |
 | Kuendeleza sekta isiyo rasmi |
 | kufanya utafiti unaotakiwa na kupanua huduma za mazao |
 | Kuendeleza na kuboresha mazao ya kilimo hasa katika zao la korosho, pamba, kahawa n.k.
kwa kutumia nguvu kazi iliyopo. |
 | Kueleza mfumo wa uthibiti wa usafirishaji wa mazao ndani ya nchi na kati ya nchi na nchi |
 | Kuhakikisha sheria ya ardhi inamsaidia kila mtu awe masikini au tajiri, mwanamke au
mwanaume na kuhakikisha kuwa sheria nyingine zinazohusiana zinamwezesha mtu kuweka dhamana
ya ardhi ili kupata mikopo. |
 | Kuhakikisha kuna sehemu za nchi zilizo nyuma zinapata msaada wa ziada unaotakiwa. |

Serikali itasaidia mahali panapohusika katika kutoa mazungumzo endelevu, huduma za
kilimo na kuwasaidia wawekezaji hodari. Malengo ya siku zijazo ni ongezeko la idadi na
ubora wa mazao ya asili na ya sasa kwa ajili ya biashara ya nje.
Viashirio (dalili)
 | Kilomita nyingi za barabara zilizokarabatiwa |
 | Ongezeko la thamani ya mazao ya kilimo |
 | Uzalishaji wa msimu wa mazao ya chakula muhimu na mazao ya biashara |
Uendelezaji wa Sekta Binafsi
Serikali imekuwa ikisaidia maendeleo ya biashara ya sekta binafsi tangu mwaka 1993 kwa
kushughulika na:
 | Sheria ya uwekezaji Tanzania |
 | Ubinafsishaji wa shughuli za biashara zilizomilikiwa na serikali |
 | Uundaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC) |
Hata hivyo, licha ya viwanda vya madini na Utalii, mwitikio wa Wawekezaji binafsi bado
haujawa mzuri.
Malengo na Shughuli
 | Kujenga upya uwezo wa kituo cha Uwekezaji Tanzania ili kutilia mkazo ukuzaji wa
uwekezaji |
 | Kuwasilisha sheria mpya za makampuni Bungeni |
 | Kuanzisha mfumo wa mafaili unaotumia kompyuta kwa ajili ya Mahakama |
 | Kuwarahisishia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuwekeza katika Tanzania (pamoja
na kulindwa kikamilifu) |
 | Kufanya mabadiliko ambayo yatapunguza gharama ya huduma za umma ikiwa ni pamoja na umeme
katika viwanda |
 | Kutekeleza kwa haraka mabadiliko muhimu ya Mbinu za Kuzuia Rushwa Kitaifa |
Serikali pia itabuni Mkakati wa kuendeleza Sekta Binafsi ifikapo kwa mwaka 2003.
Hii itasaida:
 | Kuendeleza uratibu mzuri kati ya serikali na michango ya Wafadhili |
 | Kuweka mazingira bora yanayoimarisha biashara kubwa, ndogo, ya kati na isiyo rasmi |
 | Kubadili mfumo wa kodi |
Utawala Bora
Serikali nzuri ni ile ambayo inaweza kutoa huduma bora kwa wananchi wake wote kwa
wakati wote. Pia ina utaratibu mzuri ambao unaiwezesha kukusanya fedha na kuzitumia kwa
uwazi kwa manufaa ya wananchi wote. Kwa sababu ya matumizi ya fedha kuwa wazi na dhahiri
Serikali ya aina hiyo itakuwa inawatumikia watu.
Shabaha zilizotolewa katika Mkakati wa Kuondoa Umasikini (PRSP) ni:
 | Kuendeleza utendaji kazi wa serikali katika kutoa huduma za jamii |
 | Kuendeleza njia ambazo zinawapa motisha watendaji ili kuboresha kazi |
|
Viongozi
wazuri wanapoondoka katika nafasi zao watu husema, tulifanya sisi
wenyewe.
[Tao te Ching] |
|
 | Kupunguza upotevu wa fedha na kuwa na njia ya kuwaadhibu wafanyakazi
wabadhirifu. |
Malengo:
 | Mfumo wa Serikali ambao ni madhubuti na unaofaa unawapa watu madaraka ya kujiamulia
maendeleo yao |
 | Kupunguza rushwa |
 | Kustawisha ubingwa na matumizi bora ya fedha katika mfumo wa serikali |
 | Kuimarisha uwezo wa utendaji kazi serikalini |
 | Kuimarisha uongozi wa bajeti katika ngazi ya juu na ngazi ya chini serikalini |
 | Kuunganisha Mfumo wa Taarifa za Utawala wa Fedha (IFMS) ulioundwa katika wizara zote na
Hazina ndogo. Fedha zote ambazo zinatolewa katika ngazi ya wizara ya Fedha na Hazina ndogo
zitapitia katika Mfumo wa Taarifa za Uongozi wa Fedha (IFM) na mipango yote ya matumizi na
malipo ya nyuma yatawekwa katika kumbukumbu |

| Viashirio (Dalili) |
Shughuli |
| Imarisha uaminifu na udhahiri katika uhasibu |
Imarisha mfumo madhubuti zaidi wa utawala wa fedha, udhibiti wa malipo na
matumizi, orodha ya vifaa na rasilimali na ripoti za ukaguzi |
| Bajeti zitayarishwe kwa wakati katika ngazi zote |
|
| Sekta muhimu ya utendaji kazi iliyoendelezwa na kuboreshwa |
|
| Mipango iliyoendelezwa na kukubaliwa dhidi ya rushwa katika Wizara za
Kilimo na Ushirika, Elimu na Utamaduni, Afya na Maji, ikilenga katika mbinu dhidi ya
Rushwa Kitaifa |
Fanya ukaguzi wa Mbinu za utekelezaji zilizokubaliwa na timiza mipango
dhidi ya rushwa katika Wizara za Sheria, Ujenzi, Elimu na Utamaduni, Afya, Mambo ya ndani,
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, na Mamlaka ya Mapato Tanzania |
| |
Tangaza Zabuni za Serikali katika vyombo vya Habari |
| Yaruhusu mashirika mbalimbali kutoa huduma za jamii Timiza majukumu chini
ya Programu ya Mageuzi ya Sekta za Umma |
Timiza majukumu chini ya Programu ya mageuzi ya Sekta za Umma |
| Mfumo wa Taarifa za Utawala wa Fedha (IFM) utumike katika kutengeneza
bajeti ya serikali, uhasibu na mfumo wa maelezo ya Fedha kwa ajili ya matumizi ya kawaida Bajeti
ya maendeleo iliandaliwa kwa utaratibu wa GFS |
Panua mfumo wa Taarifa za Utawala wa Fedha kwa wizara zote, idara na
wakala wa serikali Dar es Salaam na Hazina ndogo katika mikoa yote ifikapo 2002 |
Uchumi Mkuu Imara
Wakati uchumi imara unapokua, upandaji wa gharama za maisha unakuwa mdogo na serikali
inakuwa na mlingano wa mahesabu. Serikali ya Tanzania ina rekodi nzuri ya kupunguza
upandaji wa gharama za maisha na malengo kwa miaka mitatu ijayo yatajiegemeza katika hii
njia.

Malengo na Shughuli
 | Harakisha ukuaji wa uchumi (GDP) hadi asilimia 6 |
 | Upandaji wa gharama za maisha ubakie asilimia 4 |
 | Weka akiba ya serikali katika kiwango cha miezi 4 ya bidhaa zinazotoka nchi za nje na
huduma |
 | Weka mahesabu katika hali ya usawa (ongezeko la matumizi liwe dogo) |
 | Panua wigo wa kodi (na zuia ukwepaji wa ulipaji kodi) |
 | Imarisha utawala wa mfumo wa kodi |
 | Endeleza uwezo wa mameneja wa Fedha katika ngazi ya Taifa na mitaa |
Viashirio (Dalili)
 | Ukuaji wa jumla wa uchumi wa Tanzania |
 | Kiasi cha upandaji wa gharama za maisha |
 | Jumla ya rasilimali ya akiba ya kimataifa |
 | Mabadiliko katika kima cha mabadilishano ya fedha |
 | Sazo la fedha katika uchumi |
 | Ugawaji wa rasilimali ugawaji halisi wa fedha kwa ajili ya elimu, afya ya jamii,
maji, barabara za vijiji, kilimo na uzuiaji wa kuenea kwa Virusi vya UKIMWI/UKIMWI |
Matendo yafuatayo ambayo baadhi yameelezwa katika sehemu zilizotangulia katika kijitabu
hiki yatawezesha kuwa na hali imara ya uchumi
| Viashirio (Dalili) |
Matendo |
| Ukuaji wa jumla wa Uchumi wa Tanzania |
Imarisha uthabiti wa uchumi |
| Panua vitega uchumi (vya asili na vya binadamu) |
 | Imarisha barabara vijijini na huduma za miundo msingi (maji, umeme, mawasiliano n.k.) |
 | Elimisha watu katika stadi zinazotakiwa na katika kazi na utoaji ushauri |
|
| Imarisha vitega uchumi vya uzalishaji |
 | Endeleza nyenzo za uchumi mdogo |
 | Stawisha hali nzuri ya vitega uchumi ambayo inaendana na programu
 | kukuza sekta binafsi na thabiti |
 | kupunguza gharama za uendeshaji biashara |
 | kuunda mfumo wa sheria ambao ni thabiti na unaofaa |
|
|
| Endeleza Mbinu za Sekta Binafsi ifikapo mwaka 2003 |
 | Hakikisha uratibu mzuri kati ya serikali na mashirika ya wafadhili |
 | Hakikisha kuunda mazingira yanayowezesha biashara kubwa, ndogo na ya kati. Aidha kuwa na
biashara isiyo rasmi |
 | Ulipaji kodi viwango na viwango vilivyo dhibitiwa |
|
| Ukuaji wa kilimo kwa asilimia 5 ifikapo 2003 |
 | Endeleza upatikanaji wa matokeo ya tafiti za kilimo |
 | Rahisisha upatikanaji wa mikopo kwa ajili ya kilimo |
 | Kuza upatikanaji wa fedha za maendeleo vijijini, na biashara ya mazao na futa urasimi |
 | Kuza biashara ya nje ya bidhaa za kilimo · |
 | Gawa ardhi ambayo inafaa kwa umwagiliaji kwa watu masikini |
|
| Uimarishaji wa barabara za vijijini |
 | Ongeza mgao wa bajeti kwa ajili ya ukarabati na uimarishaji wa barabara za vijijini |
 | Endeleza na tumia teknolojia ya nguvukazi kwa ajili ya ukarabati na uimarishaji, na
tumia makandarasi wa nchini |
 | Imarisha uwezo wa kudhibiti ukarabati wa barabara ambazo zinajengwa na makandarasi |
|
|