kisiasa tangu katikati ya mwaka 1980, nusu ya Watanzania wote wanahofiwa kuwa masikini
na theluthi wanaishi katika ufukara mkubwa.
Lakini hali sasa inaweza kuwa inabadilika. Mwishoni mwa miaka ya 1990 serikali ilitoa
mwelekeo wa 2025 ukionyesha malengo ya muda mrefu ya kiuchumi na kijamii. Haya yalifuatwa
na Mbinu za Kitaifa za Ufutaji wa Umasikini (NPER) ambapo malengo ya ufutaji wa umasikini
hadi mwaka 2010 yalifafanuliwa. Jumuiya ya Kimataifa iliiunga mkono serikali kwa kutoa
Mbinu za Usaidizi wa Tanzania (TAS) ambapo ilieleza kwa muhtasari mbinu iliyoratibiwa
katika utoaji wa misaada. Tangu wakati huo muundo wa matumizi ya kati (MTEF) na mapitio ya
matumizi ya serikali (PER) vimetolewa. Aidha, orodha ya tathmini ya viashirio vya ustawi
na umasikini (PM) imetengenezwa.

Sasa tuna waraka wa Mkakati wa Upunguzaji wa Umasikini Tanzania (PRSP). Hii inaeleza
mbinu za muda mfupi wa kupunguza umasikini na ni sehemu ya mpango wa Nchi Masikini zenye
Madeni Makubwa (HIPC). Mbinu hii in maana kwamba serikali inapaswa kupunguza matumizi na
huku ikiruhusu shughuli za matumizi ya kuondoa umasikini kwa bajeti ya ziada na kukuza
hatua mbalimbali zisizo ingiza gharama ambazo zaweza kuondoa umasikini.
Mpango wa Mkakati wa Kupunguza Umasikini Tanzania (PRSP) ni tofauti na mipango ya awali
kwa sababu unatoa malengo thabiti na unawashirikisha watu wa kawaida. Watu wa kawaida
walihusishwa katika kutengeneza mpango huo na watahusishwa katika kuutekeleza. Na hasa
lililo muhimu ni kuwa watahusishwa katika kuhakikisha kwamba malengo yaliyobainishwa
katika mpango huo yanapatikana.
Mpango huu Uliandaliwaje?
Mwezi Oktoba 1999 kamati ya mawaziri kumi na wawili na Gavana wa Benki ya Tanzania
iliundwa kuandaa waraka wa mpango wa Mkakati wa Kupunguza Umasikini (PRSP). Kamati hii
ilisaidiwa na kamati ya wataalamu (iliratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais) ambayo
iliwahusisha maofisa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Tume ya Mipango, Wizara Kuu na Benki Kuu
ya Tanzania.
Waraka wa msingi (waraka wa awali) wa Mpango wa Mkakati wa Kupunguza Umasikini Tanzania
(PRSP)) ulitolewa kama muswada wa kwanza mwanzoni mwa mwezi Januari 2000. Waraka huu
ulijadiliwa katika mkutano wa mashauriano ambao uliwahusisha wawakilishi wa serikali na
watu waliotoka katika jumuiya ya wafadhili na makundi ya kijamii.
Waraka ulihakikiwa na kuidhinishwa na baraza la mawaziri mwanzoni mwa mwezi Februari
2000. Aidha, waraka huo ulijadiliwa na Shirika la Fedha Duniani mjini Washington mwezi
Machi 2000. Hili liliiwezesha Tanzania kuendelea na kutoa waraka kamili wa Mbinu za
Kupunguza Umasikini.
Mwezi Machi mwaka 2000 kamati ya wataalamu ilitayarisha vidokezo vya waraka wa mwanzo
kwa ajili waraka kamili wa mpango wa Mkakati za Kupunguza Umasikini Tanzania (PRSP).
Waraka huu ulijadiliwa katika warsha za kanda saba kati ya tarehe 11-12 Mei 2000. Warsha
hizi zilihudhuriwa na washiriki 804 na zilihusisha vijiji 426, madiwani 215, Wakurugenzi
wa Halmashauri 110 na watu 53 waliotoka katika mashirika yasiyo ya kiserikali. Chini ya
robo ya washiriki walikuwa wanawake. Ripoti za kila kanda zilitolewa kwa kamati ya
wataalamu tarehe 16 Mei 2000.
Mkutano wa mashauriano kati ya serikali na wafadhili uliofanywa tarehe 22 Mei 2000 na
ulifuatwa na kamati ya wataalamu ambayo ilitengeneza waraka wa mwanzo wa Mbinu za
Upunguzaji wa Umasikini Tanzania. Waraka huu ulitumia taarifa zilizotoka katika tafiti
zilizotangulia, waraka za sera na matokeo ya warsha za kanda. Tarehe 30 Juni waraka
ulijadiliwa katika mkutano ambao uliwashirikisha jumuia ya wafadhili kutoka Benki ya Dunia
na Shirika la Fedha Duniani. Tarehe 1 Julai 2000 Wabunge walijulishwa juu ya maendeleo
yaliyokwisha fikiwa na waliombwa kutoa mawazo yao.
Tarehe 3-4 Agosti 2000 kulifanyika warsha ya kitaifa ikiwa na washiriki 25 ili kupata
maoni zaidi kuhusu malengo, na kutathmini mambo muhimu ya kufanya ambayo yalikuwa
yameainishwa katika waraka wa awali. Waliohudhuria warsha hiyo ni pamoja na Makatibu
Wakuu, Wakuu wa Mikoa, Wawakilishi na Wafadhili, Mashirika ya Kimataifa, sekta binafsi,
mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, vyombo vya habari na wawakilishi wa sekta zisizokuwa
rasmi. Aidha tarehe 3 - 4 Agosti 2000 waraka wa awali ulijadiliwa na Makatibu Tawala wa
Mikoa (RAS) huko Lobo, Serengeti.
Waraka uliorekebishwa uliidhinishwa na Baraza la Mawaziri tarehe 31 Agosti 2000.
Marekebisho zaidi yalifanywa na Serikali na Shirika la Fedha Duniani/Benki ya Dunia na
Waraka wa mwisho uliidhinishwa na Bodi za Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia mwezi
Oktoba 2000.
Mipango ya baadaye itafanywaje?
Tafiti mbalimbali zinafanywa ili kupata takwimu bora za kusaidia mipango ya baadaye.
Hizi ni pamoja na: · Ukaguzi mpya wa bajeti za kaya zaidi ya 24,000 · Ukaguzi wa nguvu
kazi ili kuanzisha msingi wa soko la kazi · Sensa ya idadi ya watu na nyumba katika mwaka
2002 · Ukaguzi wa taarifa za uzazi na vifo pamoja na afya katika mwaka 2003
Kuna umuhimu wa haraka wa kuimarisha uwezo wa watu wa aina mbalimbali ili kutathmini
shughuli ambazo zimeanzishwa pamoja na waraka wa Mkakati wa Upunguzaji wa Umasikini
Tanzania (PRSP). Watu wanahitaji pia kufasili taarifa ambazo zinakusanywa na kubainishwa,
taarifa hizo zina maana gani katika masuala ya sera.
Inategemewa kuwa vikao mbalimbali vitafanywa ili kuanzisha utaratibu wa uoanishaji wa
shughuli mbalimbali katika ngazi tofauti. Aidha vikao hivi vitatafuta njia za kuhusisha
sera na ushirikishwaji wa watu. Kama ilivyoelezwa katika Mkakati wa Upunguzaji wa
Umasikini Tanzania (PRSP), Serikali imekusudia kuendeleza ushirikishaji wa watu
masikini na washika dau wengine katika utekelezaji, usimamizi na tathmini ya mbinu za
upunguzaji umasikini, na kisha kurekebisha waraka huo.