| Watu wengi masikini Tanzania wanategemea mazingira asilia kwa ajili ya
chakula chao na pia kukabili mahitaji yao kwa kuuza kuni, mkaa, asali na matunda mwitu.
Hatujui shughuli hizi kikamilifu kiasi cha kupunguza na kuweka malengo kwa ajili ya kuzuia
uharibifu wa mazingira. Taarifa zitakusanywa ili zitumike katika nakala mpya ya mpango wa
kusaidia Kupunguza Umasikini (PRSP). Utaratibu utafanywa wa kuhusisha
mipango mingine kama vile kuimarisha matumizi ya mazao yanayostahimili ukame na mpango wa
umwagiliaji unaofanywa na jamii. Aidha upandaji miti na upunguzaji wa mifugo nao pia
utahusishwa. |
| Mpangilio wa maisha unaonyesha kuwa watu masikini ambao wana mali
kidogo wanaweza kwa kutumia nguvu kidogo kuneemeka polepole kiuchumi, na kushtukia
wamerejea tena katika ufukara wao kwa sababu ya maradhi, kuachishwa kazi, kupata mazao
hafifu na wanawake kutelekezwa . Hakuna kitu kinachowazuia kuangukia katika lindi la
kukata tamaa. Na wakati wanapotumbukia huko, panaweza pasiwe na mtu yeyote anayewangoja
kuwadaka huko chini wanakoangukia. Aidha hakuna anayewapa mkono wa msaada ili waanze
upya.
[Deepa Narayan] |
|