Je, tunawezaje kusimamia kwa ukamilifu zaidi na kuona kuwa tunatekeleza tuliyokusudia?
Haja ya kuwa na Viashirio
Tunapaswa kufahamu kuwa fedha zetu zinatumika vyema. Maana yake ni kuwa inabidi tuwe na
hakika na kile tunachotaka kufanya. Aidha, tunapaswa kuangalia kama tunafaulu katika yale
tunayoyafanya.
Awali tuliona kuwa malengo yaliwekwa kwa ajili ya matendo mbalimbali ya kupunguza
umasikini. Kwa kila tendo tunapaswa kuwa na dalili (viashirio) zinazotuwezesha kupima kama
tunatekeleza malengo yetu au hapana. Serikali imeweka njia za ushauri ili kuonyesha dalili
za umasikini zinakuwaje.
Viashirio (dalili) vya aina tatu
Si rahisi kuamua mapema ni dalili zipi bora na rahisi za kutumia. Kuna aina mbalimbali
zilizo katika mfumo wa kubuni viashirio. Kimsingi, kuna aina tatu za viashirio:
Dalili za athari na matokeo
Ni za msingi na zinaweza kupima kwa urahisi uthabiti wa matendo ya mara kwa mara (kwa
mfano idadi ya watoto chini ya miaka miwili ambao wamechanjwa dhidi ya surua kila mwezi).
Dalili za kati
Zinapimwa katika kipindi cha muda mrefu. (Kwa mfano, idadi ya familia ambazo zinapata
maji safi na salama) ·
Dalili za uwakilishi
Hupima vitu vya nje vinavyowakilisha vitu vya msingi ambavyo si rahisi kupimwa (kwa
mfano, matumizi ya vifaa vya kisasa vya ujenzi wa nyumba kama njia ya mapato).

Shabaha ni kufikiria njia rahisi na viashirio bora kwa kila malengo yaliyowekwa katika
mpango. Orodha ya viashirio ambazo zimebainishwa hadi sasa zinaonyeshwa katika sura
inayofuata. Zingatia kuwa ikilazimika na ikiwezekana, maelezo yaliyotolewa kwa kuzingatia
viashirio yatueleze tofauti kati ya wanaume na wanawake na kati ya maeneo ya vijijini na
mijini.
Kujenga Mfumo wa Usimamizi na Tathmini
Muda mwingi, nguvu na fedha vinaweza kupotea kama mfumo wa ukusanyaji taarifa utakuwa
mgumu na wenye urasimu. Kazi ni kuwa watu wote wanaohusika kufikiria viashirio bora
ambavyo vinaweza kupimwa mara kwa mara na kwa urahisi.
Majukumu ya usimamizi dhidi ya umasikini yako chini ya ofisi ya Makamu wa Rais. Ofisi
hii itafanya kazi kwa ukaribu zaidi na Kitengo cha Kitaifa cha Takwimu ili kuziingiza
taarifa katika kompyuta. Kompyuta hizi zinaweka takwimu katika benki ya data za kiuchumi.
Data hizi zinaweza kutumiwa na mtu yeyote ambaye anataka kushirikishwa na anayetaka
kuzichambua. Hali hii inafanya taarifa ziwe zimeratibiwa kikamilifu.
Kwa hiyo, ni lazima tuwe tayari kukabili changamoto hii. Bado kuna udhaifu mwingi
katika kusimamia shughuli za kuondosha umasikini. Mkakati wa umasikini (PRSP) ni nafasi
nzuri ya kujenga mfumo bora na madhubuti. Kama ilivyotajwa katika mkakati huo (PRSP),
Serikali inakusudia kutafuta uwakilisho wa watu masikini na washika dau wengineo
katika utekelezaji, uangalizi na kufanya tathmini ya mbinu za kupunguza umasikini na
baadaye Kubadili Mbinu zitumikazo