
Kuza ubora wa maisha na Ustawi wa Jamii
Umasikini wa kutokuwa na mapato unatokana na elimu ndogo, afya mbaya na ustawi wa jamii
ambao ni wa mashaka. Kwa ujumla, inaonekana wazi lipi linahitaji kutendwa bali itachukua
muda kugundua vipengele vyote vinavyohitajiwa. Aidha itachukua muda pia kujua gharama
inayotakiwa. Mipango ifuatayo imekwisha buniwa:-
| Mpango wa Taifa wa Mbinu za uendelezaji Elimu ya Msingi |
Ifikapo Julai 2001 |
| Mpango wa Taifa wa Mbinu za uendelezaji Kilimo |
Ifikapo Juni 2001 |
| Mpango wa Taifa wa Mbinu za uendelezaji Vijiji |
Ifikapo Desemba 2001 |
Programu ya mageuzi ya Serikali za Mitaa imekwishaanza kutekelezwa katika wilaya zote.
Hii inasaidia Serikali za Mitaa kutekeleza huduma muhimu.
Mipango hii itaruhusu:
 | Majengo chakavu na huduma dhaifu kurekebishwa (Serikali za Mitaa zitaamua mahali pa
kujenga majengo mapya) |
 | Misaada mbalimbali ipatikanayo toka kwa wafadhili na hivyo kuwa nje ya bajeti (serikali
itafanya kazi ya uratibu na wafadhili) |
 | Upunguzaji wa umasikini utagharimu pesa nyingi zaidi kuliko ilivyo sasa (serikali
itashughulikia upatikanaji zaidi wa fedha) |

Elimu
Shabaha kuu ni kuwa na elimu zaidi na bora zaidi. Hii itajumuisha ufutaji wa ujinga
ifikapo mwaka 2010. Aidha inakusudia kuleta uwiano sawa kati ya wasichana na wavulana
katika shule za msingi na sekondari ifikapo mwaka 2005.
Malengo
| |
Hadi kufikia 2003 |
| Uandikishaji wa wanafunzi shuleni kijumla |
Hadi kufikia 85% |
| Kiwango cha wanaoacha shule |
Toka 6.6% hadi 3% |
| Uandikishaji wa wanafunzi kihalisi |
Toka 57% hadi 70% |
| Wanafunzi wanaoshinda mtihani wa darasa la 7 |
Toka 20% hadi 50% |
| Wanafunzi wanaoingia sekondari |
Toka 15% hadi 21% |
| Mipango ya Elimu ya Watu Wazima |
Iongezeke |
Shughuli
 | Upimaji wa mshule na uendelezaji wa mipango utafanywa |
 | Serikali itagharimia gharama za muhimu za shule za msingi (hasa mishahara ya walimu) |
 | Ada za shule zitafutwa ifikapo Julai 2001 |
 | Shule zitaendelezwa kwa kupatiwa vitabu, vifaa, madawati, vyoo, vyumba vya madarasa,
nyumba za walimu, n.k. |
 | Uwiano thabiti kati ya wanafunzi walimu utatumiwa |
 | Walimu wataendelezwa na kuhamasishwa |
 | Kitengo cha ukaguzi kitaimarishwa |
 | Shule binafsi na elimu ya jumuiya (ikiwa pamoja na elimu ya watu wazima) itaimarishwa. |
Viashirio (dalili)
 | Ongezeko halisi la kiwango cha uandikishaji wanafunzi katika elimu ya msingi |
 | Ongezeko halisi la wanafunzi wanaoanza shule |
 | Ongezeko halisi la wanafunzi wanaosoma darasa la saba |
 | Ongezeko halisi la wanaoshinda mtihani wa darasa la saba |
|
| Mwanadamu anakuwa mwanadamu kwa sababu ya wanadamu wengine
[Methali ya Kiafrika] |
|
Afya
Umri wa kuishi unapungua (hasa kwa sababu ya ugonjwa wa UKIMWI). Lengo ni kuongeza umri
hadi kufikia miaka 52 ifikapo 2010. Hili litawezekana kwa kuboresha lishe na kuwa na
huduma bora za afya pamoja na maji salama.
Malengo
|
Ifikapo mwaka 2003 |
| Kiwango cha vifo vya watoto wachanga |
Toka 99 hadi 85 kwa kila watoto 1000 |
| Chini ya umri wa miaka 5 |
Toka 158 hadi 127 kwa kila watoto 1000 |
| Vifo vya akina mama wakati wa kujifungua |
Toka 529 hadi 450 kwa kila watoto 1000 |
| Vifo kutokana na malaria kwa watoto chini ya miaka 5 |
Toka 12.8 hadi 10 % |
| Watu wanaopata maji salama |
Toka 48.5 hadi 55% |
| Uchanjwaji wa watoto chini ya miaka 2 dhidi ya surua, dondakoo
na pepopunda |
Toka 71 hadi 85% |
| Wilaya ambazo zina kampeni dhidi ya UKIMWI |
Hadi kufikia 75% |
| Punguza hali ya kudumaa |
Toka 43.4 hadi 20% |
| Punguza upotevu |
Toka 7.2 hadi 2% |
| Wafanyakazi wenye taaluma ya uzazi |
Toka 50 hadi 80% |
| Tekeleza kikamilifu sera ya maji ya mwaka 2000 kama
inavyotakiwa |
|
Shughuli
 | Ongeza kiwango na imarisha ugawaji wa fedha za serikali kwa ajili ya afya ya jamii |
 | Toa afya bora karibu na mahali wanapoishi watu wote wa mijini na vijijini |
 | Hakikisha misaada inatolewa kwa afya za jamii kwa kuimarisha vituo vya afya na hospitali
na kubadili mfumo wa utendaji wa kazi |
 | Imarisha mfumo wa kutoa misaada kwa wafanyakazi, madawa na vifaa vingine vya afya |
 | Tekeleza programu ya udhibiti wa malaria kama ilivyopangwa kati ya mwaka 2000/01 hadi
2002/03 |
 | Kuza sekta binafsi na shirikisha makundi ya jumuiya katika utoaji wa huduma za afya |
VIRUSI VYA UKIMWI/UKIMWI
| Kuza utambuzi wa ugonjwa wa UKIMWI na afya ya jamii pamoja na
wanafunzi kufundishwa mashuleni |
| Uchungu na huzuni huja kwa kuangalia uwapendao wakifa kwa sababu ya
kukosa fedha za matibabu na hali hii ni upeo wa juu wa matatizo ya umasikini unaokuja
kimya kimya
[Deepa Narayan] |
|

Lishe
Kuza elimu ya lishe, hasa kwa akina mama na imarisha afya ya uzazi na mpango wa uzazi
Anzisha programu ya mfuko wa fedha wa shule
Maji
 | Ongeza matumizi ya serikali katika huduma za maji vijijini |
 | Tathmini mahitaji ya makundi tofauti ya watu vijijini |
 | Imarisha vianzo vya maji na data za maji salama |
 | Fanya ukaguzi wa upimaji maji |
 | Fanya ukaguzi wa mara kwa mara wa ubora wa huduma za maji na tumia vipimo vya shirika la
Afya Duniani (WHO) |
 | Kuza uvunaji maji ya mvua |
 | Karabati mipango yote ya usambazaji maji ambayo haifanyi kazi. Aidha karabati vifaa vya
kutoboa udongo |
 | Imarisha sheria, kanuni na taratibu za kuhifadhi maji katika vyanzo vya maji |
 | Zipe uwezo Serikali za Mitaa na jumuiya kulinda vyanzo vya maji |
Viashirio (Dalili)
 | Watoto wachanga na viwango vya vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano |
 | Asilimia ya watoto ambao wamepata chanjo kamili baada ya mwaka mmoja |
 | Uwiano wa wilaya zenye kampeni za utambuzi wa UKIMWI |
|
| Afya inahusisha mwili mzima, akili, na ustawi wa jamii na si tu
kutokuwa mgojwa na kutojiweza.
[Shirika la Afya Duniani WHO] |
|
 | Uwiano wa kaya ambazo zinapata maji salama |
Ustawi wa Jamii Kushiriki katika shughuli za Siasa
Kati ya vitu vingine ambavyo vinahusiana na ustawi wa jamii ni kuhusu kushiriki katika
maamuzi ya kisiasa yanayohusu maisha yako, na kujiona wanalindwa na sheria na kanuni.
Pametokea maendeleo mazuri katika eneo hili katika miaka mitatu iliyopita na mengi
yanapangwa.
Serikali imekuwa wazi katika shughuli inazofanya na imekuwa sikivu kwa watu wa kawaida.
 | Watu wa kawaida sasa wanaweza kujua serikali inatumiaje fedha zao na kushiriki katika
mikutano inayoamua sera zipi zifuatwe na serikali |
 | Magazeti, Redio, Televisheni vinaeleza watu wa kawaida mambo yanayoendelea |
 | Kuna Jumuiya hiari za Wananchi ambazo hutoa mchango na changamoto |
 | Serikali za Mitaa zitapewa uwezo zaidi wa kuamua yapi yatekelezwe katika mikoa yao baada
ya kutekeleza Programu ya Mageuzi ya Serikali za Mitaa. |
Linapozingatiwa suala la sheria na taratibu, watu lazima wajione salama kutembea
mitaani, kuweza kutumia mahakama, na kujua kuwa mfumo wa serikali ni thabiti, wa haki na
uko wazi. Mipango ifuatayo inafanywa katika kiwango cha Serikali za Mitaa:
Malengo
 | Tekeleza kikamilifu njia za Kupunguza Umasikini kama zilivyopangwa |
 | Tekeleza kikamilifu Programu ya Mageuzi ya Serikali za Mitaa ifikapo mwaka 2003 katika
wilaya zote |
 | Hakikisha ushirikishwaji wa washika dau wote katika kuunda, kutekeleza na kutathmini
mipango yote ya maendeleo |

Shughuli
 | Kuza mfumo wa usalama wa jamii |
 | Karabati majengo ya mahakama za mwanzo na vifaa vya jumuiya |
 | Ajiri mahakimu ili kesi zilizoko katika mahakama za Mwanzo ziweze kuamuliwa mapema |
Katika Kiwango cha Taifa:
| |
Hadi mwisho wa mwaka 2003 |
| Uwiano wa vikao vilivyopangwa vya Mahakama za Rufaa na vile vilivyotimizwa |
Toka 50% hadi 100% |
| Uamuzi wa Mahakama |
Uharakishwe |
| Uwiano wa kesi zilizoamuliwa na zile zilizoletwa |
Toka 63% hadi 80% |
| Wastani wa muda uliotumiwa katika kuamua kesi za biashara |
Zipunguzwe hadi miezi 18 |
Kutakuwa pia na uchunguzi wa rushwa katika :
 | Wizara ya Sheria |
 | Wizara ya Ujenzi, Elimu, Afya na Mambo ya Ndani na ofisi zao za Mikoani na Wilayani |
 | Ofisi ya Mwanasheria Mkuu |
 | Mamlaka ya Mapato Tanzania |
Viashirio (Dalili)
Viashirio vya ushirikishwaji:
 | Idadi ya washiriki na ushiriki katika warsha za mashauriano |
 | Ushiriki wa makundi ya jumuiya |
 | Usambazaji wa ripoti za serikali |
Ripoti za kila miezi minne kuhusu maendeleo ya mageuzi ya mfumo wa mahakama na
uchunguzi wa rushwa. |