
Uchumi Mkuu Imara (Macroeconomic Stability) ni matokeo ya kuwa na kodi
ya hazina, sera za fedha na kiwango cha kubadilishana fedha inayokusudia kufikia malengo
ya uchumi mkuu kama vile ukuaji wa uchumi, kupanda kwa gharama za maisha, madeni ya nje na
akiba halisi ya kimataifa.
Uchumi Mdogo (Microeconomics) ni elimu kuhusu jinsi viwanda, sekta
fulani, biashara au kaya zinavyofanya kazi.
Jumla ya Pato la Taifa (Gross Domestic Product - GDP) ni kipimo cha
jumla ya pato la utajiri ambalo linapatikana nchini katika muda maalum. Kwa maneno mengine
Pato la Taifa ni tathmini ya bidhaa zote na huduma ambazo zinaundwa na zinabadilishwa kwa
fedha. Kama jumla ya thamani ya bidhaa na huduma mwaka huu ni asilimia 1% zaidi kuliko ya
mwaka jana basi ukuaji wa pato la utajiri ni asilimia 1%. Lakini jumla ya pato la taifa
(GDP) huacha kazi zingine za thamani ambazo zingeweza kujumuishwa kwa mfano,
uendeshaji wa kaya na familia kwa kupata nishati rahisi na maji, na pia watu kujenga
nyumba zao kwa kutumia vifaa vya asilia na ustawishaji wa vyakula kwa ajili ya matumizi
yao.
Jumla ya Pato la Taifa (GNP) ni sawa na jumla ya pato la taifa lakini
unaongezea biashara ya ndani na biashara ya nje.
Ukuaji Halisi (Real Growth): Kwa vipengele vyote viwili jumla ya pato
la utajiri (GDP) na ukuaji wa pato la utajiri (GNP), kama ukuaji ni asilimia 7% kwa mwaka,
lakini mfumuko wa bei umekuwa asilimia 5% basi Ukuaji Halisi ungekuwa asilimia 2% tu kwa
mwaka.
Mfumuko wa Bei (Inflation): Kipimo cha kupanda kwa bei kati ya mwaka
mmoja na mwaka unaofuata hasa ukizingatia wazo la kupata vifaa vya madukani/sokoni.
Mtaji wa jamii (Social Capital) ni kama gundi
inayounganisha pamoja familia, makundi na jumuiya. Inahusisha imani, desturi na tabia za
jamii ambazo husaidia kufanya kazi pamoja kwa uthabiti katika makundi yaliyo rasmi na
yasiyo rasmi.
Vyama vya Jumuiya (Civil Society Organisation):Inahusisha vyama rasmi
ambavyo vimesajiliwa na serikali na vile visivyo rasmi. Vyama hivyo ni pamoja na vile vya
hisani, dini, vya shughuli maalumu, kundi shawishi, kitaaluma, na vyama vya makundi
maalumu kama vile vyama vya wafanyakazi na vyama vya wanafunzi. Vyama visivyo rasmi ni
pamoja na Upatu, vyama vya makabila, mpira wa miguu ambavyo vinaundwa na vijana wa kiume
na netiboli vinavyoundwa na vijana wa kike.
Matayarisho Ya Bajeti inayozingatia maskini (Pro-poor Budgeting): na
usimamizi wa matumizi (and expenditure monitoring). Fedha zinatengwa katika bajeti kwa
ajili ya programu zinazowalenga watu masikini. Lakini fedha hizi zinapaswa kupitia Hazina,
wizara inayohusika, serikali za Mikoa na Halmashauri za Wilaya/ Miji na kitengo cha huduma
(k.m. shule au hospitali) kabla ya mtu masikini kupata faida. Kwa usimamizi thabiti fedha
hizi zinaweza kutumika vizuri.
Mapitio ya Matumizi ya Serikali (Public Expenditure Review). Timu ya
Matumizi ya Serikali hukutana mara moja kila baada ya majuma mawili ili kutafakari jinsi
serikali inavyopata na kutumia fedha zilizo kwenye bajeti. Timu hii iliundwa mwaka 1997
inawajumuisha viongozi wakuu wa serikali na wawakilishi kutoka katika jumuiya ya
wafanyabiashara, makundi ya jumuiya na makundi ya wafadhili wa nje.

Bajeti za Serikali (Government Budgets). Serikali ni kama familia
ambayo inapaswa kuweka uwiano kati ya fedha zinazoingia na fedha zitumikazo. Kama hakuna
fedha zinazoingia serikali inapaswa kuamua itumie kiasi gani na isitumie kiasi gani.
Utaratibu wa kukusanya taarifa hii na kufanya uamuzi ndiyo huitwa Bajeti
Njia za Mapato ya Serikali (Source of government income):