Shukurani
Home Dibaji Yaliyomo Sura ya 1 Sura ya 2 Sura ya 3A Sura ya 3B Sura ya 3C Sura ya 4 Sura ya 5 Maana ya maneno Vifupisho Maswali Shukurani

 

Back to Hakikazi

 

SHUKRANI

Mawazo ya kuchangia juhudi za namna ya kuelimisha Umma kuhusu mkakati wa kupunguza umaskini Tanzania kwa lugha rahisi yalitokana na juhudi za pamoja ndani ya Shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Hakikazi Catalyst. Shirika hili linaongozwa na Emmanuel Kallonga ambae alishawahi kufanya kazi serikalini na kwa mara ya mwisho akiwa Mwakilishi wa Shirika la Oxfam UK nchini Tanzania. (www.hakikazi.org)   Shirika la Hakikazi Catalyst ni mshiriki katika Mtandao wa Kupunguza Madeni na Kusukuma Maendeleo (TCDD).

Uandishi kwa lugha nyepesi kwa kiingezeza umefanywa na George Clark, Mtaalam Mshauri wa vyama vya jumuiya vya jamii. Mtaalamu huyo amejihusisha na maendeleo ya kimataifa toka mwaka 1974 na kwa sasa ni mtendaji mkuu wa Shirika la Caledonia Centre for Social Development  (www.caledonia.org.uk)  

Tunawashukuru kwa dhati wasomaji wote wa Dar es Salaam na Arusha waliojitolea kusoma rasimu ya awali ya kijitabu hiki kwa mchango wao uliosaidia kusahihisha hadi ikaeleweka.

Hakikazi Catalyst inamshukuru sana Ally Masoud (kipanya@hotmail.com ) kwa mchango wake na uwezo wake wa pekee kwa kuchora katuni zilizofanya kijitabu kieleweke kwa urahisi.

Tunawashuku pia Dr. Y.I. Rubanza na Prof. H. Mwansoko kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa kufasiri kijitabu hiki kwa kiswahili rahisi ili kiweze kueleweka zaidi.

Aidha tunatoa shukrani kwa Mtandao wa Kupunguza Madeni na Kusukuma Maendeleo (TCDD) kwa mchango wao wa kukisambaza kijitabu hiki.

Hatuna budi kuwashukuru pia watendaji wa kitengo cha kuondoa umasikini katika Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kututia moyo katika kazi hii. Tunatambua kuwa Serikali ikishirikiana na vyama hiari vya maendeleo ya jamii katika kupambana na umasikini, mafanikio yatapatikana.

Mwisho tunalishukuru Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID)  (www.dfid.gov.uk) kwa kugharamia uchapishaji wa kijitabu hiki.

 

 

Back ] Home ]